Je,Kisukari Kinasababisha Ganzi, Viungo Kuwaka Moto Na Kukatwa Vidole Au Mguu?

Mungu Ni Upendo

Je, Kisukari Kinasababisha Ganzi, Viungo Kuwaka Moto Na Kukatwa Vidole Au Mguu?
UGONJWA WA DIABETIC NEUROPATHY
Bila shaka umeshamwona mtu aliyekatwa vidole au mguu kwa sababu ya kisukari. Katika mada yetu ya leo tutalijadili tatizo linalotokana na kisukari ambalo husababisha watu kukatwa viungo na matatizo mengine mengi kama viungo kufa ganzi au kuwaka moto. Tatizo hili kiutaalamu huitwa diabetic neuropathy.
Diabetic neuropathy ni namna ya uharibifu wa neva unaotokana na mtu kuwa na kisukari. Uwepo wa sukari (glucose) kwa wingi ndani ya damu unaweza kuharibu neva za sehemu mbalimbali za mwili wako. Lakini mara nyingi diabetic neuropathy huharibu neva za kwenye nyayo na miguu.
DIABETIC PERIPHERAL NEUROPATHY NERVE DAMAGE(KUHARIBIKA KWA NEVA)
Kutokana na neva ambazo zimeharibiwa, dalili za diabetic neuropathy zinaweza kuwa ni maumivu na kufa ganzi kwenye miguu na nyayo, matatizo ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, mkondo wa mkojo (urinary tract,) mishipa ya damu na moyo. Watu wengine hupata dalili ndogo lakini kwa wengine huweza kuwaletea maumivu makali au kuwafanya washindwe kufanya kazi.
Diabetic neuropathy ni tatizo la kawaida linalojitokeza baada ya mtu kuwa na kisukari. Unaweza kuzuia diabetic neuropathy au kupunguza makali yake kwa kudhibiti kiwango chako cha sukari na kufuata mtindo wa kimaisha unaoilinda afya yako.
DALILI ZA DIABETIC NEUROPATHY
Kuna aina kuu nne za diabetic neuropathy. Unaweza ukatatizwa na aina moja au na zaidi ya aina moja ya neuropathy. Dalili zitategemea aina ya neuropathy na ni neva zipi zilizoathirika. Kama kawaida, dalili huanza taratibu na unaweza usigundue lo lote hadi neva zinafikia kuharibika kwa kiwango kikubwa.
PERIPHERAL NEUROPATHY
Hii ni aina ya diabetic neuropathy inayoonekana zaidi. Huanza kwa kuathiri nyayo na miguu, kisha mikono na viganja. Dalili zake huonekana zaidi usiku, nazo zinaweza kuwa:
DIABETIC PERIPHERAL NEUROPATHY IN LEGS
1. Ganzi na kupungua kwa usikivu wa maumivu au mabadiliko ya joto
2. Kuhisi misisimko au viungo kuwaka moto
3. Maumivu makali au kukakamaa misuli
4. Kuzidi kwa usikivu wa kugusa – kwa wengine hata uzito wa shuka huwaumiza
5. Udhaifu wa misuli
6. Kupoteza ushiriakiano wa viungo
7. Matatizo makubwa ya miguu, vidonda, maumivu ya maungio ya mifupa na mifupa.
DIABETIC NEUROPATHY GANGRENE
AUTONOMIC NEUROPATHY
Autonomic nervous system huongoza shughuli za moyo, kibofu cha mkojo, tumbo, utumbo, viungo vya uzazi na macho. Kisukari huweza kuathiri neva katika eneo lo lote katika haya, na kusababisha:
1. Hali ya kushindwa kutambua kuwa kiwango cha sukari kimeshuka (hypoglycemia unawareness)
2. Matatizo ya kibofu cha mkojo, pamoja na maambukizi kwenye njia ya mkojo au kushindwa kutoa au kuumaliza mkojo kutoka kwenye kibofu (urinary retention) au kushindwa kuuzuia mkojo (incontinence)
3. Kufunga choo na/au kuharisha
4. Kupungua kwa kasi ya utoaji wa chakula kutoka kwenye tumbo (gastroparesis) na kusababisha kichefuchefu, kutapika, kucheua na kukosa hamu ya kula
5. Matatizo katika kumeza
6. Kuongezeka au kupungua kwa jasho
7. Mabadiliko ya jinsi macho yanavyozoea mabadiliko ya kutoka kwenye mwanga hadi gizani
8. Kuongezeka kwa mapigo ya moyo wakati wa mapumziko
9. Kushuka ghafla kwa pressure baada ya kuketi au kusimama kunakoweza kusababisha kuzimia
10. Uume kushindwa kusimama au kusimama ukiwa legelege
11. Ukavu ukeni
12. Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa.
RADICULOPLEXUS NEUROPATHY (DIABETIC AMYOTROPHY)
Radiculoplexus neuropathy inaathiri neva za kwenye mapaja, nyonga, matako au miguu. Huonekana zaidi baina ya waathirika wa kisukari cha Type 2 na watu wenye umri mkubwa. Aina hii ya neuropathy huitwa pia amyotrophy, femoral neuropathy au proximal neuropathy.
DIABETIC AMYOTROPHY
Dalili huonekana zaidi upande mmoja wa mwili, ingawa huweza kusambaa na upande wa pili. Unaweza kuwa na:
1. Maumivu makali kwenye paja na nyonga au tako yanayodumu siku nzima au zaidi
2. Baadaye udhaifu na kusinyaa kwa misuli ya paja
3. Ugumu kunyanyuka baada ya kuketi
4. Kuvimba tumbo
5. Kukonda
MONONEUROPATHY
Mononeuropathy au focal neuropathy ni kuharibika kwa neva fulani iliyo usoni, katikati ya mwili (torso) au mguuni. Mononeuropathy mara nyingi humpata mtu ghafla na huweza kuambatana na maumivu makali sana. Lakini , mara nyingi haileti madhara ya kudumu.
Dalili mara nyingi huondoka bila tiba yo yote baada ya wiki au miezi kadhaa. Dalili hutofautiana kulingana na neva iliyoharibiwa. Unaweza kupata maumivu sehemu za:
1. Unyayo au katikati ya goti na ankle
2. Sehemu ya chini ya mgongo au nyonga
3. Sehemu ya mbele ya paja
4. Kifua au tumbo
Mononeuropathy huweza vile vile kusababisha matatizo ya neva kwenye macho na uso, na kuleta:
1. Matatizo katika kuona vitu vizuri
2. Kuona vitu viwiliviwili
3. Kuwashwa nyuma ya jicho moja
4. Kupooza upande mmoja wa uso (Bell’s palsy)
Wakati mwingine mononeuropathy hutokea pale kitu kinapogandamiza juu ya neva. Carpel tunnel syndrome ni aina moja ya nephropathy itokanayo na mgandamizo kwa watu wenye kisukari. Inaweza kusababisha ganzi au msisimko mkononi au kwenye vidole, isipokuwa kidole cha mwisho. Mkono unaweza kuwa dhaifu, na kuangusha vitu.
CHANZO CHA DIABETIC NEUROPATHY
KUHARIBIKA KWA NEVA NA MISHIPA YA DAMU
Chanzo kamili hutofautiana kulingana na aina ya neuropathy. Watafiti wanafikiria kuwa baada ya muda, sukari ambayo haikudhibitiwa huharibu neva na kuziondolea uwezo wake wa kutuma taarifa (signals), na kuleta diabetic neuropathy. Sukari nyingi katika damu vile vile hudhoofisha kuta za mishipa midogo ya damu (capillaries) inayoleta oksijeni na virutubishi kwenye neva.
DIABETIC PERIPHERAL NEUROPATHY
Muunganiko wa sababu huweza kuleta uharibifu wa neva, zikiwemo:
. Kuvimba kwa neva kunakotokana na kushambuliwa na kinga za mwili. Kinga za mwili kwa bahati mbaya hushindwa kuzimbua neva (huzifikiria ni vitu kutoka nje vyenye madhara) na kuzishambulia
. Sababu za kiurithi ambazo hazihusiani na kisukari zinaweza kuwasababishia baadhi ya watu kupata uharibifu wa neva
. Matumizi ya tumbaku na pombe huharibu neva na mishipa ya damu na kuongeza uwezekano wa kushambuliwa na wadudu.
MATATIZO YATOKANAYO NA DIABETIC NEUROPATHY
Kuna madhara makubwa yanayoweza kutokana na diabetic neuropathy, ikiwa ni pamoja na:
. Kupoteza dole gumba, nyayo au mguu.
Kuharibika kwa neva kunaweza kukufanya ushindwe kuzisikia nyayo zako. Mikwaruzo au kujikata kwenye nyayo kunaweza kulifanya eneo hilo kupata maambukizi na taratibu jeraha likageuka kuwa kidonda kikubwa. Hata mikwaruzo midogo isiyopona baadaye huwa madonda. Hali ikiwa mbaya zaidi, maambukizi husambaa hadi kwenye mifupa, na vidonda kusababisha kufa kwa tishu (gangrene). Kukatwa kwa dole gumba, unyayo au sehemu ya chini ya mguu huwa sasa ni lazima.
DIABETIC NEUROPATHY MADHARA YAKE
1. Uharibifu wa maungio ya mifupa. Uharibifu wa neva unaweza kusababisha maungio ya mifupa kupotea ubora wake, na kuleta hali iitwayo Charcot joint. Hii kwa kaida hutokea kwenye maungio ya mifupa madogo ya kwenye mguu. Dalili ni kukosa hisi na kuvimba kwa sehemu hizo za maungio, wakati mwingine kuharibika kwa umbo la joint.
2. Mambukizi ya njia ya mkojo na kutokwa mkojo ovyo. Neva zinazosimamia utendaji wa kibofu cha mkojo zikifa, unaweza ukashindwa kuutoa mkojo wote kutoka kwenye kibofu. Bakteria huweza kujijenga ndani ya kibofu cha mkojo na figo, na kusababisha maambukizi ya njia ya mkojo. Uharibifu wa neva unaweza pia kuathiri uwezo wako wa kutambua kuwa unahitaji kukojoa au kudhibiti misuli inayoruhusu mkojo utoke, na kusababisha kuvuja kwa mkojo (incontinence).
3. Kutotambua uwingi wa sukari.
4. Kushuka kwa pressure kwa ghafla. Kuharibika kwa neva zinazosimamia mtiririko wa damu kunaweza kuathiri uwezo wa mwili wa kurekebisha pressure. Hii inaweza kusababisha kushuka kwa ghafla kwa pressure unaposimama baada ya kuwa uliketi (orthostatic hypotension), na kukufanya usikie kizunguzungu na ukazimia.
5. Matatizo ya mmeng’enyo wa chakula.
6. Kushindwa kumudu tendo la ndoa. Autonomic neuropathy mara nyingi huharibu neva zinazoathiri viungo vya uzazi. Wanaume wanaweza kupata tatizo la uume kushindwa kusimama. Wanawake wanaweza kupata tatizo la uke kuwa mkavu au kutosikia hamu ya kufanya mapenzi.
7. Kutotoka au kutoka jasho jingi. Uharibifu wa neva unavuruga utendaji kazi wa tezi za jasho na kuufanya mwili wako kushindwa kudhibiti kiwango chake cha joto ipaswavyo. Baadhi ya watu wenye autonomic neuropathy wanatoa jasho kwa wingi sana, na hasa usiku au wakati wakila chakula. Jasho kidogo au kutotoka jasho (anhidrosis) kunaweza kuhatarisha maisha.
TIBA YA DIABETIC NEUROPATHY
Hakuna dawa inayojulikana kuponya diabetic neuropathy. Tiba inayotolewa inalenga:
1. Kupunguza kasi ya ugonjwa
2. Kuondoa maumivu
3.. Kudhibiti matatizo yatokanayo na ugonjwa na kurudisha utendaji wa viungo.
SOMA HAPA>>>Tiba Ya Kisukari
Wasiliana Nami David Mondi-Mshauri Toka Green World


HUDUMA NI SAWA NA BURE KABISA.
KUMBUKA,Tuna Wajibu Wa Kujali Afya Zetu Wenyewe Katika Dunia Ya Sasa Kabla Ya Kuugua.Inawezekana Kuwa Salama.
Sms call Whatsapp 0654523177
Email afyaraha@gmail.com

Huku Ndo Kwa BabaLao, Green World-AfyaRaha
www.afyaraha.com

Comments